19 Sep 2024 / 86 views
Suarez atundika daruga rasmi

Maisha ya Luis Suarez ya miaka 17 ya Uruguay yalifikia kikomo walipotoka sare tasa dhidi ya Paraguay katika mechi ya kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia la Amerika Kusini.

Suarez, 37, alitangaza Jumatatu kwamba anastaafu kutoka kwa majukumu ya kimataifa.

Anamaliza kama mfungaji bora wa muda wote wa Uruguay akiwa amefunga mabao 69 katika mechi 143 tangu alipocheza kwa mara ya kwanza dhidi ya Colombia Februari 2007.

Suarez na familia yake walikusanyika uwanjani kabla ya kuanza kwa hafla ya kabla ya mchezo, ikijumuisha salamu za mashabiki na ujumbe wa video kutoka kwa gwiji wa Argentina na mchezaji mwenzake wa Inter Miami Lionel Messi.

"Uruguay ni kubwa kuliko mchezaji yeyote. Kuanzia kesho nitakuwa shabiki mwingine," aliuambia umati.